Deuteronomy 25:13-16

13 aUsiwe na mawe ya kupimia ya aina mbili katika mkoba wako, moja zito na jingine jepesi. 14 bUsiwe na vipimo viwili tofauti katika nyumba yako, kimoja kikubwa, kingine kidogo. 15 cNi lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako. 16 dKwa maana Bwana Mungu wako humchukia yeyote ambaye hufanya mambo kama haya, yeyote anayetenda kwa udanganyifu.

Copyright information for SwhNEN